IQNA

Nakala ya Qur'ani yenye uzito wa kilo 154 yaonyeshwa Madina +PICHA

18:20 - July 22, 2017
Habari ID: 3471079
TEHRAN (IQNA)-Nakala kubwa ya Qu'rani Tukufu yenye uzito wa kilo 154 imeonyeshwa katika mji mtakatifu wa Madina.

Nakala hiyo ya Qur'ani Tukufu imewekwa katika maonyesho yaliyo karibu na Msikiti wa Mtume Mtukufu SAW (Al-Masjid an-Nabawi) na watu wote wako huru kutembelea maonyesho hayo.

Kwa mujibu wa Hamza Abdul Karim, afisa katika maonyesho hayo, nakala hiyo ya Qur'ani Tukufu iliandikwa na kutayarishwa na raia wa Afghanistan, Gholam Muhiyiddin miaka 200 iliyopita.

Katika wakati huo, kutokana na uzito wake, nakala hiyo ya Qur'ani Tukufu ilibebwa na ngamia wanne kutoka Afganistan hadi Madina.

Kwa mujibu wa Abdul Karim, katika maonyesho hayo, kuna nakala zingine nadra za Qur'ani katika maonyesho hayo, zikiwemo zilizoandikwa katika ngozi. Halikadhalika maonyesho hayo yana Qur'ani zilizotarjumiwa kwa lugha mbali mbali za dunia.

Nakala ya Qur'ani yenye uzito wa kilo 154 yaonyeshwa Madina +PICHA


Nakala ya Qur'ani yenye uzito wa kilo 154 yaonyeshwa Madina +PICHA

3621250

captcha