IQNA

Waislamu Palestina wapinga upekuzi wa Israel katika Msikiti wa al Aqsa

6:17 - July 25, 2017
Habari ID: 3471084
TEHRAN (IQNA)-Taasisi za Kiislamu Palestina zimechukua hatua za pamoja kupinga vizingiti vilivyowekwa na utawala wa Kizayuni wa Israel katika Msikiti wa al-Aqsa.

Sheikh Omar al-Kiswani, mkurugenzi mkuu wa Msikiti wa al-Aqsa katika mji wa Quds (Jerusalem) ametuma ujumbe wa sauti na kusema, "Msimamo wa Shirika la Waqfu, wanazuoni wa Kiislamu na wasimamizi wa Al Aqsa ni kupinga hatua za utawla wa Kizayuni katika Msikiti wa al-Aqsa na kutokubali milango ya kielekroniki katika msikiti huo.”

Katika ujumbe huo al-Kiswani amesisitiza kuwa, Wapalestina hawatakubali mabadiliko yoyote katika milango na pia kamera eti za usalama zilizowekwa na Wazayuni katika msikiti huo.

Tangu Ijumaa ya Julai 14 mwezi huu hadi Jumapili iliyopita, wanajeshi wa utawala haramu wa Israel waliufunga Msikiti wa al-Aqsa kwa amri ya Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa Israel na hivyo kuwazuia waumini kwenda kutekeleza ibada ya Swala katika eneo hilo takatifu. Hata baada ya kufungua tena milango ya msikiti huo, wanajeshi hao waliweka vizingitina vituo vya upekuzi mkali unaoambatana na udhalilishaji dhidi ya waumini wanaotaka kuingia katika kibla hicho cha kwanza cha Waislamu kwa ajili ya ibada.

Hujuma hiyo ya Israel dhidi ya Masjid al-Aqswa imefuatiwa na ghadhabu na hasira za Wapalestina. Hata hivyo, malalamiko hayo ya Wapalestina yamejibiwa kwa risasi na mtutu wa bunduki. Wapalestina kadhaa wameshauawa shahidi na mamia ya wengine kujeruhiwa katika ukandamizaji huo.

3622432

captcha