IQNA

Qarii Mashuhuri wa Qur’ani Uturiki aaga dunia

0:38 - July 26, 2017
Habari ID: 3471086
TEHRAN (IQNA)-Qarii (msomaji) mashuhuri wa Qur’ani Tukufu nchini Uturuki, Sheikh Abdullah Hatipoglu aliaga dunia Jumapili akiwa na umri wa miaka 88.

Marehemu Hatipogulu alikuwa qarii katika Msikiti wa Jamia wa Al Fatih katika mji wa Istanbul nchini Uturuki na alipitisha umri wake akiihudumia Qur’ani Tukufu na pia kutangaza dini tukufu ya Kiislamu.

Katika taarifa kufuatia kuaga dunia Sheikh Hatipolgu, Jumuiya ya Kimataifa ya Maulamaa Waislamu (IUMS) imetoa taarifa na kusema: "Tumepokea habari za kuaga dunia ndugu yetu, Sheikh Abdullah Hatipolgu, kwa nyoyo zilizojaa Imani kuhusu aliyoyakadiria Allah SWT.”

Taarifa hiyo imeongeza kuwa, Sheikh Hatipoglu alipitisha umri wake akitoa mafunzo ya Qur’ani ambapo kwa muda wa miaka 55 alikuwa akuhudumu katika Msikiti wa Al Fatih na Msikiti wa Sultan Ahmad mjini Istanbul.

Sheikh Hatipoglu alizikwa Jumapili mjini Istanbul katika mazishi yaliyoongozwa na Katibu Mkuu wa IUMS Ali al-Qaradaghi.

Qarii Mashuhuri wa Qur’ani Uturiki aaga dunia

623039

captcha