IQNA

Inna Lillah wa Inna Ilahyi Rajioun

Msomaji mashuhuri wa Qur’ani Misri, Sheikh el-Tantawi ameaga dunia

0:30 - July 27, 2017
Habari ID: 3471089
TEHRAN (IQNA)-Qarii (msomaji) mashuhuri wa Qur’ani Tukufu kutoka Misri, Sheikh Mohammad Abdul Wahhab el-Tantawi ameaga dunia akiwa na umri wa zaidi ya miaka 70.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, Sheikh el-Tantawi, ambaye ni maarufu kwa qiraa yake iliyojaa hisia, aliaga dunia mapema Jumatano baada ya kuugua ugonjwa wa moyo kwa muda mrefu.

Sheikh el-Tantawi ambaye pia alikuwa Hafidh wa Qur’ani Tukufu alianza qiraa yake kitaalamu mwaka 1969 baada ya kuanza masomo katika Chuo Kikuu cha Al Azhar. Baadaye alianza kusoma Qur’ani katika radio za eneo la Delta nchini Misri katika muongo wa 1980.

Sheikh Tantawi alikuwa mashuhuri katika n katika nchi nyingi za Waislamu duniani na katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran anakumbwa na wengi alipoitembelea nchi hii mwaka 2009.

Baraza Kuu la Qur’ani nchini Iran limetuma salamu za rambirambi kufuatia kuagad dunia qarii huyu mtajika na aliyebobea katika taaluma ya kusoma Qur’ani.

Mazishi ya marehemu Sheikh el-Tantawi yanafanyika Alhamisi katika kijiji alikozaliwa karibu na mji wa Mansour, mji mkuu wa mkoa wa Dakahlia kaskazini mwa Misri.

Katika mahojiano maalumu na mwandishi wa IQNA, Ustadh Taha Mohammad Abdul Wahab ambaye pia ni qarii mtajika nchini Misri amefafanua kuhusu kifo cha Sheikh Tantawi na kusema: "Jumatano asubuhu 26 Julai, Sheikh el-Tantawi alirejea kwa Mola wake akiwa nyumbani kwake. Umri wa kila mwanadamu uko mikononi mwa Mwenyezi Mungu. Takribani siku nne zilizopita, marehemu Sheikh el-Tantawi alisoma Qur’ani katika Msikiti wa Sayyida Nafisa mjini Cairo wakati wa Alfajiri. Katika siku za hivi karibuni alionekana mwenye kuchoka sana.” Ustadh Tahad Mohammad Abdul Wahab anaongeza kuwa: "Katika kipindi cha siku mbili zilizopita alipata maumivi shadidi ya moyo na tatizo hilo liliendelea hadi alipoaga dunia Jumatano.”

Skiliza tilawa ya Marehemu Sheikh el-Tantawi hapo chini

3623496


captcha