IQNA

Nchi zenye idadi kubwa zaidi ya Mahujaji

10:15 - August 23, 2017
Habari ID: 3471138
TEHRAN (IQNA)-Kila mwaka mamilioni ya Mahujaji kutoka kila kona ya dunia humiminika katika Mji Mtakatifu wa Makka kwa ajili ya Ibada ya Hija.

Kwa mujibu wa mafundisho ya Kiislamu, Hija ni ibada ya faradhi ambayo kila Mwislamu mwenye uwezo wa kifedha na kimwili anapaswa kutekeleza mara moja katika umri wake.

Mwaka huu inatarajiwa kuwa kutakuwa na mahujaji milioni 1.3 kutoka nchi mbali mbali duniani huku kukiwa na mahujaji wengine 567,000 kutoka ndani ya Saudi Arabia.

Kwa mujibu wa Idara ya Hija Saudi Arabia, Indonesia ndio nchi yenye idadi kubwa zaidi ya Mahujaji mwaka huu wa 1438 Hijria sawa na 2017 Miladia. Inatazamiwa kuwa Waindonesia 221,000 watatekeleza ibada ya Hija mwaka huu. Indoneisa iko Kuisni Mashariki mwa Asia na ina idadi ya watu milioni 261 na hivyo kuifanya kuwa nchi ya Kiislamu yenye idadi kubwa zaidi ya watu duniani. Nchi zingine zenye idadi kubwa ya Mahujaji ni Pakistan (179,210), India (170,000), Bangladesh (128,000), Nigeria (95,000) na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran (86,500).Nchi zenye idadi kubwa zaidi ya Mahujaji

Kwa mujibu wa tangazo la wakuu wa Saudi Arabia, Agosti 23 ni siku ya kwanza ya mwezi wa Dhul Hijja mwaka 1438 na Hija inatazamiwa kuanza rasmi Agsoti 30 huku Siku Kuu ya Idul Adha ikitazamiwa kuwa Ijumaa Septemba Mosi.

3632845

captcha