IQNA

Papa ataka Myanmar iheshimu haki za Waislamu wa Rohingya

18:59 - August 28, 2017
1
Habari ID: 3471145
TEHRAN (IQNA)-Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani ameitaka Mynmar iheshimu haki za jamii ya Waislamu wa kabila la Rohingya.
Papa Francis ameeleza kusikitishwa na mashambulizi hayo dhidi ya Waislamu wa Rohingya wa nchini Mynamar na kusema kuwa: Watu wote wanapaswa kusaidia ili kufanikisha kukomeshwa mashambulizi na hatua za ukandamizaji dhidi ya Waislamu wa Myanmar.

Aidha amesisitiza kuhusu kusitishwa mashambulizi na utumiaji mabavu dhidi ya Waislamu wa kabila la Rohingya huko Myanmar.

Waislamu karibu 100 wa kabila wa Rohingya wameuawa katika kipindi cha siku kadhaa zilizopita wanaoishi katika mkoa wa Rakhine huko Myanmar kufuatia kushadidi mashambulizi ya jeshi la nchi hiyo.
Waislamu wa Myanmar pia wamekuwa wakishambuliwa na Mabuddha wenye misimamo mikali na wanajeshi wa Myanmar dhidi ya Waislamu wa Rohingya katika mkoa wa Rakhine magharibi mwa nchi hiyo tangu miaka kadhaa iliyopita hadi sasa yamesababisha kuuliwa na kujeruhiwa maelfu ya Waislamu hao na kuwafanya makumi ya maelfu ya wengine kuwa wakimbizi. Waislamu wa Rohingya wamekuwa wakikandamizwa kwa miaka kadhaa sasa huku wakinyimwa haki zao za msingi.

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa Waislamu wa kabila la Rohingya ni jamii ya wachache duniani inayodhulumiwa na kunyongeshwa zaidi. Serikali ya Myanmar inakataa kuwapa haki za uraia Waislamu hao ambao idadi yao ni zaidi ya watu milioni moja na laki tatu.

Katika miaka ya karibuni, Waislamu wengi wa kabila la Rohingya nchini Myamnar wameuawa au kulazimika kuhama makazi yao na kuwa wakimbizi katika nchi za Thailand, Malaysia na Indonesia kutokana na mashambulio ya Mabuddha wenye misimamo ya kufurutu mpaka wanaoungwa mkono na serikali ya nchi hiyo.

3463768

Kishikizo: iqna rohingya waislamu papa
Imechapishwa: 1
Inatathminiwa: 0
Haiwezi kuchapishwa: 0
allyul akbar
0
0
Innalillah wainna illayh rjn
captcha