IQNA

Madrassah 4,000 za Qur'ani Nigeria zajumuishwa katika mfumo rasmi wa elimu

11:05 - September 12, 2017
Habari ID: 3471168
TEHRAN (IQNA)-Serikali ya Jimbo la Sokoto nchini Nigeria imezijumuisha madrassah 4,000 za Qur'ani katika mfumo rasmi wa elimu.

Kamishna wa Elimu ya Msingi na Sekondari katika jimbo hilo Dakta Jabbi Kilgori ametoa tamko hilo Jumapili wakati akikagua madrassah za Qur'ani katika eneo la Bodinga jimboni hapo na kuongeza kuwa mradi huo utasimamiwa na kamati ya viongozi wa jadi wakiongozwa na Sultan wa Sokoto Al Haji Sa'ad Abubakr.

Ameongeza kuwa kamati hiyo itahgakikisha kuwa watoto wanaoingia katika shule katika jimbo hilo wanapata mafunzo ya Qur'ani na pia masomo mengine ya shule kama vile hesabu, kemia, fizikia na biolojia.

Afisa huyo amesema mradi huo unaungwa mkono na Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Watoto UNICEF ili kukabiliana na idadi ndogo ya watoto wanaojiunga na shule za kiserikali jimboni humo. Wazazi wengi katika jimbo la Sokoto lenye Waislamu wengi wamekuwa wakifadhilisha kuwapelekea watoto katika Madrassah za Qur'ani kutokana na kukosekana mafunzo ya Qur'ani katika shule za kawaida za serikali. Aidha kumekuwepo na sababu zingine za kijamii, kiutamaduni na kiuchumi pia hupelekea watoto wasijiunga na shule za serikali.

3463884


captcha