IQNA

Mama, watoto wake mapacha wahifadhi Qur’ani kikamilifu

12:06 - September 19, 2017
Habari ID: 3471183
TEHRAN (IQNA)-Mama Muirani na watoto wake mapacha wamefanikiwa kuhifadhi Qur’ani kikamilifu.

Bi. Twahira Rahimi, na watoto wake mapacha,Rayhana na Amir Mohammad, wamehifadhi Qur’ani Tukufu kikamilifu baada ya masomo katika Kituo cha Qur’ani cha Haram Takatifu ya Abdul Adhim Hassani AS katika eneo la Rey, kusini mwa Tehran.

Mama huyo mwenye umri wa miaka 35 anasema alipata ilhamu kutoka kwa hafidh mashuhuri wa Qur’ani nchini Iran Sayyed Mohammad Hussein Tabatabai, aliyezaliwa mwaka 1991 na kupata taufiki ya kuhifadhi Qur’ani Tukufu kikamilifu akiwa na umri wa miaka mitano. Anasema wakati alipojaaliwa kuzaa watoto mapacha mwaka 2005, aliamua kuwafunza kuhifadhi Qur’ani Tukufu huku yeye binafsi pia akiwa anaendelea na jitihada za kuhifadhi Kitabu hicho Kitakatifu.

Anaongeza kuwa walijisajili katika Kituo cha Qur’ani cha Haram Takatifu ya Abdul Adhim Hassani AS ambapo iliwachukua wote watatu miaka sita kuweza kuhifadhi Qur’ani kikamilifu. Bi. Twahira Rahimi anasema kuhifadhi Qur’ani kumewasaidia watoto wake mapacha kuweza kuboresha masomo yao ya kawaida shuleni. Aidha anasema: "Tutajitahidi kutekeleza mafundisho ya Qur’ani katika muda wote wa maisha yetu, Inshalllah.”


3638331
captcha