IQNA

Msomi wa Ahul Sunna nchini Lebanon

Mwamko wa Imam Hussein AS umejengeka katika msingi wa Qur'ani

16:02 - September 23, 2017
Habari ID: 3471188
TEHRAN (IQNA)-Mwanazuoni wa ngazi za juu wa Ahlul Sunna nchini Lebanon amesema mwamko wa Imam Hussein AS dhidi ya utawala wa kiimla na kidhalimu wa Yazid.

Katika mahojiano maalumu na IQNA, Sheikh Ghazi Hunaina, mwanazuoni aliye katika mji wa Sidon na ambaye ni mwenyekiti wa harakati ya kisiasa ya al-Nahdha amesema mwamako wa Imam Hussein AS ulikuwa mwito kwa madhehebu zote za Kiislamu kusimama na kupinga udhalimu na ukandamizaji.

Ameongeza kuwa harakati ya Imam Hussein AS ilikuwa na lengo na kutetea haki na uadilifu kwa msingi wa mafundisho ya Qur'ani Tukufu na Sira ya Mtume Muhammad SAW.

Sheikh Hunaina amesema mwamko wa Ashura una masomo na ibra kwa kila mtu na moja kati ya mafunzo muhimu ni kutetea haki na kumuamini Mwenyezi Mungu.

Amesema Ummah wa Kiislamu uanapaswa kutekekeleza kivitendo mafunzo yaotokanayo na mwamko wa Imam Hussein katika kukabiliana na madola ya kibeberu na njama zao dhidi ya Waislamu.

Sheikh Hunaina aliitaja Marekani na utawala wa Kizayuni kuwa Mayazidi wa zama hizi ambao wanatekeleza njama dhidi ya Waislamu ikiwa ni pamoja na kuanzisha makundi ya kigaidi kama vile ISIS na Al Nusra. Aidha mwanazuoni huyo wa Ahul Sunnah nchini Lebanon amesisitiza kuwa, mwamko wa Imam Hussein AS haufungamani na kundi au madhehebu maalumu bali ni mwamko wenye kuwaongoza wanadamu wote kuelekea katika haki.

Itakumbukwa kuwa miaka 1378 iliyopita kulingana na kalenda ya Hijria, moja kati ya vita mashuhuri katika historia ya Kiislamu na ya mwanadamu, vilitokea baina ya majeshi ya haki na batili katika ardhi ya Karbala huko Iraq. Siku hii inajulikana kwa jina la Ashura ambayo ni siku ya 10 ya Mwezi wa Muharram. Katika siku hiyo mjukuu wa Mtume Muhammad SAW, Imam Hussein bin Ali bin Abi Twalib AS, alisimama kishujaa na wafuasi wake waaminifu 72, kukabiliana na jeshi la batili la Yazid bin Muawiya ili kuilinda dini ya Allah.

Hamasa ya Karbala ilikuwa dhihirisho la mambo mawili makuu. Kwanza ni ujasiri, ushujaa, moyo wa kujitolea, uaminifu pamoja na kuyapokea kwa moyo mkunjufu mauti ya kuuawa shahidi katika njia ya Mwenyezi Mungu, sifa walizojipamba nazo wapiganaji wachache wa jeshi la haki wakiongozwa na Imam Hussein AS dhidi ya Yazid bin Muawiya. Pili ni upeo wa ukatili, udhalimu na unyama ulioonyeshwa na jeshi batili la Yazid bin Muawiya. Baada ya kupambana kishujaa, hatimaye mjukuu huyo wa Mtume Muhammad SAW aliuawa shahidi yeye, watoto, ndugu zake na masahaba zake katika siku hiyo ya Ashura.

3463984

captcha