IQNA

Jeshi la Myanmar lamuua mtoto aliyekuwa amehifadhi Qur'ani

11:41 - December 20, 2017
2
Habari ID: 3471317
TEHRAN (IQNA)-Katika kuendeleza ukatili dhidi ya Waislamu, wanajeshi wa Myanmar wamemkamata mtoto aliyekuwa amehifadhi Qur'ani na kisha kumuua katika jimbo la Rakhine.

Taarifa zinasema mtoto huyo alishikiliwa kwa siku kadhaa na baada ya hapo kuuawa pasina maafisa wa usalama kubainisha sbabu ya ukatili wao na kisha kiwiwili chake kukabidhiwa familia yake.

Wakazi wa eneo hilo wanasema yamkini mtoto huyo alikamatwa kwa sababu ya kushukiwa kuhusika katika kile kinachodaiwa kuwa eti ni kitendo cha uhalifu na haikutarajiwa angeuawa.

Mtoto huyo aliyekuwa na umri wa miaka 12 alikuwa amebakia na familia yake katika kijiji cha Nurula mjini Maungdaw katika jimbo la Rakhine baada ya aghalabu ya wakazi Waislamu wa eneo hilo kutafuta hifadhi katika nchi jirani ya Bangladesh.

Siku ya Jumanne, shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch lilichapisha ripoti ya mauaji ya makusudi ambayo yamekuwa yakitekelezwa na jeshi la Myanmar katika jimbo la Rakhine.

Jeshi la Myanmar na Mabudha wenye misimamo mikali wamekuwa wakiteketeza moto vijiji vya Waislamu katika jimbo la Magharibi la Rakhine tokea Novemba mwaka jana. Waislamu wamekuwa wakiuawa kiholela, wanawake kunajisiwa na maelfu kujeruhiwa katika kile Umoja wa Mataifa umekitaja kuwa ni 'mauaji ya kimbari."

Wimbi hilo la mauaji lilishika kasi kuanzia Agosti 25 ambapo taarifa zinasema katika kipindi cha mwezi mmoja tokea wakati huo, Waislamu zaidi ya 6,500 wameuawa na wengine karibu laki saba kukimbilia katika nchi jirani ya Bangladesh.

Imechapishwa: 2
Inatathminiwa: 0
Haiwezi kuchapishwa: 0
Salumsaid
0
0
Wasione wanatumaliza dunia nzima tutaungana kulipa dhurma hiyo
Bila jina
0
0
imeniuma xana xiku ya kiama ikifika ipo adhabu kali xana
captcha