IQNA

Nakala Milioni 1.6 za Qur’ani Zachapishwa Iran katika kipindi cha miezi tisa

0:33 - January 06, 2018
Habari ID: 3471344
TEHRAN (IQNA)-Zaidi ya nakala milioni 1.6 za Qur’ani Tukufu zimechapishwa katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika kipindi cha miezi tisa iliyopita.

Akizungumza na IQNA, Bw. Azizullah Mortadhawi, wa kitengo cha uratibu  katika Taasisi ya Darul Qur’an  Karim amesema, idadi kamili ya nakala za Qur’ani zilichochapishwa kaunzia Machi 21 2017 ni milioni 1.606. Amesema uchapishaji nakala za Qur’ani Tukufu umeongezeka nchini Iran kwani katika kipindi mshabaha mwaka jana idadi ya nakala hizo ilikuwa ni milioni .1529

Taasisi ya  Darul Qur’an Karim inayosimamia uchapishaji Qur’ani nchini Iran inafungamana na Shirika la Ustawi wa Kiislamu nchini Iran. Taasisi hiyo pia ndio ambayo hutoa vibali vya uchapishaji wa Qur’ani.

3678969

captcha