IQNA

Binti Muislamu ahujumiwa Canada, Hijabu yake yararuliwa

10:38 - January 13, 2018
Habari ID: 3471352
TEHRAN (IQNA)-Nchini Canada, binti Muslamu mwenye umri wa miaka 11 ameshambuliwa na Hijabu yake kuraruliwa wakati akiwa njiani kuelekea shuleni katika tukio la hujuma ya chuki dhidi ya Waislamu.

Msemaji wa polisi katika mji wa Toronto amesema, mwanaume aliyetekeleza hujuma hiyo alijaribu mara mbili katika kipindi cha dakika 10, kukata hijabu ya binti huyo kwa makasi wakati akielekea shuleni akiwa ambeandamana na kaka yake siku ya Ijumaa.. "Nilichanganyikiwa, niliingiwa na wasi wasi na kupata hofu kubwa," amesema Khawlah Noman ambaye yuko katika darasa la sita amewaambia waandishi habari.

"Nilipiga mayowe na mtu huyo akakimbia. Tulifuata umati wa watu ili kuepuka shari yake lakini alitufuata na aliendelea kuikata hijabu yangu tena."

Bodi ya Shule katika Wilaya ya Toronto imesema imesikitishwa na hujuma huyo huku Waziri Mkuu wa Jimbo la Ontario Kathleen Wynne akilaani hujuma hiyo na kusema haiwakilishi fikra za watu wa jimbo hilo.

Hadi sasa hakuna aliyekamatwa kufuatia hujuma dhidi ya binti huyo Muislamu.

Tukio hilo linajiri huku ikikaribia mwaka moja tokea gaidi mwenye chuki dhidi ya Uislamu alipouhujumu Msikiti wa Mji wa Quebec na kuwua Waislamu sita walipokuwa wakiswali.

Pamoja na hayo hivi karibuni  Waziri Mkuu Justin Trudeau alisema Waislamu nchini Canada wamekuwa na mchango mkubwa na ni rasilimali muhimu kwa nchi.

3464929

captcha