IQNA

IUMS yalaani kukandamizwa kukandamizwa wanazuoni Waislamu Saudia, UAE

14:34 - January 20, 2018
Habari ID: 3471362
TEHRAN (IQNA)-Jumuiya ya Kimataifa ya Wanazuoni Waislamu (IUMS) imelaani tawala za Saudi Arabia na Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) kwa kuendelea kuwashikilia kinyume cha sheria wahubiri wa Uislamu.

TEHRAN (IQNA)-Jumuiya ya Kimataifa ya Wanazuoni Waislamu  (IUMS) imelaani tawala za Saudi Arabia na Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) kwa kuendelea kuwashikilia kinyume cha sheria wahubiri wa Uislamu.

Katika taarifa IUMS imelaani vikali kushiliwa pasina kufunguliwa mashtaka wanazuoni hao na imetaka waachiliwe huru mara moja kwani hakuna kosa walilofanya sipikuwa tu walibainisha wazi mitazamo yao.

Taarifa hiyo imetolwa baada ya kuenea habari kuwa ya kulazwa hospitalini Salman al-Ouda, mmoja wa shakhsia wakubwa wa upinzani na kidini nchini Saudi Arabia ambaye miezi minne iliyopita, alitiwa mbaroni kwa amri ya Mohammed bin Salman, Mrithi wa Kiti cha Ufalme na Waziri wa Ulinzi wa nchi hiyo.

Taarifa iliyotolewa Alhamisi na Abdullah Al-Ouda, mtoto wa kiume wa Sheikh Salman al-Ouda, kiongozi wa kidini na muballigh mashuhuri nchini Saudia aliyetiwa mbaroni baada ya kukosoa siasa mbovu za Mohammed Bin Salman, imesema kuwa hali ya baba yake huyo aliyekamatwa na maafisa usalama wa Saudia mwezi Septemba mwaka jana imeendelea kuwa mbaya.

Jumuiya ya Kimataifa ya Wanazuoni Waislamu  iliasisiwa mwaka 2004 na ina makao yake makuu nchini Qatar.

Katika miezi ya hivi karibuni utawala wa Saudi Arabia umekuwa ukikumbwa na misukosuko mingi na katika jaribio la kuzima malalamiko, utawala wa Riyadh umekithirisha ukandamizaji wa wapinzani kwa kutumia mkono wa chuma.

3683233/

captcha