IQNA

Msikiti wahujumiwa The Hague, Uholanzi

22:06 - February 04, 2018
Habari ID: 3471380
TEHRAN (IQNA)-Watu wasiojulikana wameuhujumu na kuharibu msikiti katika mji wa The Hague nchini Uholanzi.

Hakuna kundi lololote lilolodia kuhusuka na kitendo hicho cha Ijumaa ambapo pia bendera ya Uturuki iliyokuwa msikitini hapo imebandikwa maandishi yaliyo dhidi ya Rais Recep  Tayyip Erdogan wa Uturuki.

Akizungumza na waandishi habari,  Bw. Sinasi Koc, mkuu wa Msikiti wa Ahi Evran, ambao ungali unaendelea kujengwa  amelaani vikali hujuma hiyo na kusema yamkini inahusiana na oparesheni ya kijeshi ya Uturuki dhidi ya Wakurdi katika mji wa Afrin nchini Syria.

Ameongeza kuwa, "kuna wale ambao hawataki kuona tukiwa na umoja na mashikamano ambao wanataka kuleta vurugu miongoni mwetu. Hawatafanikiwa kwani Allah yuko nasi."

Msikiti uliohujumiwa unasimamiwa na Wakfu wa Kiislamu nchini Uholanzi.

Operesheni za jeshi la Uturuki katika mji wa Afrin katika mkoa wa Aleppo, kaskazini mwa Syria zilianza Januari 20 na hadi sasa bado zinaendelea. Katika operesheni hizo zinazozishirikisha ndege za kivita na vifaru, hadi sasa makumi ya watu wameuawa na wengine wengi kujeruhiwa.

Uturuki inasema kuwa, operesheni zake katika eneo hilo zina lengo la kukabiliana na wanamgambo wa Kikurdi wanaopata himaya ya Marekani. Serikali ya Syria inapinga oparesheni hiyoa ya Uturuki na kuitaja kuwa uvamizi wa kijeshi unaolenga kuvuruga mamlaka yake ya kujitawala.

3688394

captcha