IQNA

Mashindano ya Qur'ani ya Kuwait Yaanza

10:13 - April 12, 2018
Habari ID: 3471462
TEHRAN (IQNA)-Mashindano ya 9 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Kuwait, maarufu kama Zawadi ya Kuwait, yalianza Jumanne katika mji mkuu wa nchi hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa mashindano hayo ya Qur'ani Tukufu yanatazamiwa kuendelea hadi Aprili 10 na kuna washiriki 138 kutoka nchi 79.

Akizungumza katika sherehe za ufunguzi, Waziri wa Wakfu na Masuala ya Kiislamu Kuwait, Sheikh Fahd al Afasi amesema amshindano hayo yana vitengo mbali mbali vya kuhifadhi Qur'ani na pia mashindano katika qiraa.

Lengo kuu la mashindano hayo ya Qur'ani ya Kuwait limetajwa kuwa ni kuwapa motisha wasomaji na waliohifadhi Qur'ani kwa njia bora zaidi duniani.

Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inawakilishwa katika mashindano hayo na Mohammad Javad Delfani katika kitengo cha kuhifadhi Qur'ani Tukufu kikamilifu na Mehdi Gholamnejad katika qiraa.

3704699

captcha