IQNA

Jeshi la Syria laukomboa mji wa Douma na eneo zima la Ghouta Mashariki

13:45 - April 13, 2018
Habari ID: 3471463
TEHRAN (IQNA)-Jeshi la Syria limeukomboa mji wa Douma; mji wa mwisho huko Ghouta ya Mashariki kuwa chini ya udhibiti wa magaidi wanaopata himaya ya kigeni

Mji huo umekombolewa katika kipindi cha chini ya miezi miwili tangu jeshi la Syria lianzishe oparesheni ya kuwafurusha magaidi katika mji huo karibu na mji mkuu wa Syria Damascus.  

Meja Jenerali Yuri Yevtushenko Mkuu wa Kituo cha Amani na Suluhu cha Russia huko Syria amesema Alhamisi kuwa bendera ya Syria iliyopeperushwa katika jengo moja katika mji wa Douma ni ishara kwamba jeshi la Syria linadhibiti eneo hilo na Ghouta yote ya Mashariki. Eneo la Ghouta ya Mashariki limekuwa likitumiwa na magaidi kama kituo chao cha kuanzishia mashambulizi dhidi ya raia na miundombinu mbalimbali huko Damascus. Inafaa kuashiria hapa kuwa jeshi la Russia limekuwa likiipatia Syria msaada wa ndege za kivita katika oparesheni yake dhidi ya magaidi iliyoanza Februari 19 mwaka huu.

Wakati huo huo, Jeshi la Syria limetangaza kuwatia mbaroni wanajeshi kadhaa wa Uingereza  kufuatia oparesheni iliyoanza kutekelezwa na jeshi  huko Ghouta ya Mashariki tangu tarehe 26 Februari mwaka huu kwa lengo la kuwaangamiza magaidi katike eneo hilo na kuwasaidia wananchi wa Syria. 

Wakati huo huo, leo Maelfu ya wakazi wa eneo la Douma, Ghouta Mashariki nchini Syria wamemiminika mabarabarani kusherehekea kutimuliwa magaidi wanaofuata idolojia ya Uwahabi wanaoitwa 'Jeishul-Islami' kutoka eneo hilo ambalo kwa muda mrefu lilikuwa mikononi mwa magaidi hao wakufurishaji.

Inafaa kuashiria hapa kuwa, kwa mara nyingine na kupitia mbinu za kizamani zilizochakaa, Marekani imeituhumu serikali ya Damascus kwamba imetumia silaha za kemikali katika eneo la Ghouta Mashariki la mkoa wa Rif Dimashq, na hivyo kutishia kuishambulia kijeshi nchi hiyo. Hii ni katika hali ambayo Rais Donald Trump wa Marekani na katika kulegeza kamba kuhusu msimamo wake wa huko nyuma ya kutaka kuishambulia Syria, jana Alkhamisi aliandika katika mtandao wa kijamii wa Twitter kwamba: "Kamwe sijawahi kusema ni muda gani tutaishambulia Syria." Aidha jeshi la serikali ya Syria limeendelea kupambana na magaidi hususan katika kambi za Yarmouk, iliyoko kusini mwa mji mkuu Damascus.

3465531

captcha