IQNA

Mashindano ya Qur'ani ya wanafunzi wa shule Denmark

12:39 - April 20, 2018
Habari ID: 3471473
TEHRAN (IQNA)-Mashindano ya usomaji Qur'ani Tukufu maalumu kwa wanafunzi wa shule yamefanyika katika mji mdogo wa Glostrup ulio karibu na mji mkuu wa Denmark, Copenhagen.

Mashindano hayo yalifanyika Jumatano ambapo washindi walitunikiwa zawadi punde baada ya mashindano kumalizika

Mashindano hayo ya siku moja yalifanyika katika Msikiti wa Fateh unaofungamana na Jumuiya ya Vituo vya Kiislamu ya Denmark.

Mkuu wa Jumuiya hiyo, Ilyas Kokcu akihutubu katika mashindano hayo alisisitiza kuwa kushinda au kushika nafasi ya kwanza si lengo la mashindano bali nia ni kuimarisha ufahamu wa Qur'ani Tukufu.

Aidha alitoa wito kwa wazazi Waislamu wawafunzo watoto wao msingi wa Qur'ani wa kuwa na maadili mema si kwajili ya faida za kidunia tu bali pia kwa ajili ya kesho Akhera.

Waislamu wanakadiriwa kuwa asilimia tano ya watu wote milioni sita nchini Denmark.

3465590

 

captcha