IQNA

Washiriki 44 katika Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ya wanachuo nchini Iran

18:24 - April 24, 2018
Habari ID: 3471479
TEHRAN (IQNA)-Washiriki 44 wamefuzu katika fainali ya Mashindano ya 6 ya Kimataifa ya Qur'ani ya Wanafunzi Waislamu katika vyuo vikuu vya nchi mbali mbali duniani.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, kati ya washiriki hao 44,  wasomaji Qur'ani (quraa) ni 19 na walihofidahi Qur'ani Tukufu kikamilifu (hufadh) ni 25.

Sayyed Ali Akbar Shamsian mkuu wa tawi la mkoa wa Khorassan Razavi la Jumuiya ya Harakati za Qur'ani ya Wanaakademia wa Iran inayofungamana na Akademia ya Elimu, Utamaduni na Utafiti Iran (ACECR)  amesema nchi 35 kutoka mabara ya Asia, Afrika, na Ulaya zinawawakilishi katika mashindano hayo. Amesema Mashindano hayo yatafanyika Mashhad kuanzia Aprili 26-29.

Sayyed Shamsian ameongeza kuwa, mashindano hayo yatakuwa na majajsi sita kutoka Iran na wane kutoka nchi za kigeni. Aidha mashindano hayo ni sehemu ya Mashindano ya 35 ya Kimataifa ya Qur'ani ya Iran ambayo yalianza  Alhamisi iliyopita mjini Tehran ambayo pia yanajumuisha  mashindano ya wanawake, ya wenye ulemavu wa macho, na ya wanachuo wa vyuo vya kidini.

Jumuiya ya Harakati za Qur'ani ya Wanaakademia wa Iran inayofungamana na Akademia ya Elimu, Utamaduni na Utafiti Iran (ACECR) imekuwa ikiandaa mashindano ya Qur’ani ya wanafunzi Waislamu baada ya kila miaka miwili tokea mwaka 2006 kwa lengo la kuimarisha umoja na ushirikiano baina ya wanafunzi Waislamu kote duniani sambamba na kustawisha kiwango cha harakati za Qur’ani katika vyuo vikuu.

Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ya Iran, ambayo yanafanyika katika miji mitatu ya Tehran, Mashhad na Qum, ni tukio kubwa zaidi linalohusiana na Qur'ani katika Ulimwengu wa Kiislamu na yamekuwa yakiimarika kila mwaka.

h3708640  

captcha