IQNA

Msikiti wahujumiwa Scotland, vipande vya nugruwe vyatupwa mlangoni

11:06 - May 03, 2018
Habari ID: 3471492
TEHRAN (IQNA)- Watu wanaouchukua Uislamu na Waislamu wanauhujumi msikiti huko Scotland nchini Uingereza na kutupa vipande vya nyama ya nguruwe mlangoni.

Hujuma hiyo imeripotiwa Jumamosi usiku wiki hii katika Kituo cha Kiislamu na Msikiti wa Dunfermline na tayari polisi imeanzisha uchunguzi.

Katika taarifa kupitia ukurasa wa Facebook, wakuu wa msikiti huo wamesema hujuma hiyo ilikuwa kitendo cha kuwalenga kwa makusudi ambao dini yao imeharamisha nguruwe.

Taarifa hiyo imesema jamii ya Waislamu imekuwa ikiendesha  jitihada za kuoneysha uzalendo na kuishi ka maelewano huko Scotland na kusisitiza kuwa aghalabu ya watu wa eneo hilo wamewaonyesha Waislamu ukarimu na uungaji mkono.

Aidha wakuu wa msikiti huo wamesema chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu imekuwa ikichochewa kupitia mitandao ya kijamii na kwa msingi huo kuna haja ya serikali za kieneo na kitaifa kuchukua hatua kukabiliana na tatizo hilo. Aidha wamesistiza kuwa wanaoeneza chuki na hofu katika jamii ni wachache na hivyo kuna haja ya ushirikiano kukabiliana na tatizo hilo. Halikadhalika  wamesisitiza kuwa Uislamu ni dini ya amani inayopinga misimamo mikali.

Kanisha la Scotland limetoa taarifa na kulaani hukuma hiyo ya msikiti na kusema wakaazi wa Dunfermline wanaisho kwa amani na kwamab kanisa litawaunga mkono majirani Waislamu. Polisi wamesema wataimarisha doria katika maeneo ya karibu na msikiti katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

3465701

captcha