IQNA

Watu 17 wauawa katika hujuma ya kigaidi msikitni nchini Afghanistan

11:46 - May 07, 2018
Habari ID: 3471499
TEHRAN (IQNA)- Watu wasiopungua 17 wameuawa Jumapili kufuatia mlipuko wa bomu katika msikiti ambao ulikuwa pia unatumika kama kituo cha kuwasajili wapiga kura katika mkoa wa Khost kusini mashariki mwa Afghanistan.

Maafisa wa usalama wanasema mlipuko huo ulisababishwa na bomu ambalo liliachwa ndani ya msikiti na watu wasiojulikana. Mkuu wa Idara ya Afya mkoani Khost Habib Shah Ansari amethibitsha kupoteza maisha watu 17 na kujeruhiwa wengine 34 katika tukio hilo.

Hakuna kundi lolote ambalo limedai kuhusika na hujuma hiyo ambayo ni sehemu ya msururu wa mashambulio ambayo yamelenga vituo vya kuwasajili wapiga kura tangu zoezi hilo lianza kitaifa kote Afganistan mwezi Aprili.

Kundi la kigaidi la Taliban ambalo limekuwa likiwaonya watu wasijiandikishe kupiga kura limetoa taarifa na kukanusha kuhusika na hujuma hiyo. Msemaji wa Taliban Zabiullah Mujahid amedai kuwa shambulizi hilo limetekelezwa na maadui ambao wanataka kuliharibia jina kundi lake.

Mwezi jana karibu watu 60 waliuawa katika hujuma ya kigaidi iliylenga kituo cha kuwasajili wapiga kura katika mji mkuu, Kabul, ambapo kundi la kigaidi la ISIS lilidai kuhusika.

Uchaguzi wa bunge nchini Afghanistan umepengwa kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu katika hatua ambayo inatahtminiwa kuwa muhimu katika mchakato wa kutafuta amani ya kudumi nchini humo.

Magaidi wakufurishaji wanatekeleza jinai nchini Afghanistan pamoja na kuwepo wanajeshi wa Marekani na shirika la kijeshi la NATO nchini humo kwa muda wa miaka 16 sasa ambao waliihujumu nchi hiyo yenye utajiri mkubwa wa mali asili kwa madai ya kupambana na ugaidi. Mbali na hayo tokea wanajeshi hao wa kigeni, wakiongozwa na Marekani, walipoivamia Afghansitan mwaka 2003, uzalishaji mihadarati umeongezeka maradufu nchini humo.

3465740

captcha