IQNA

Al Azhar kuandaa mashindano ya Qur'ani kwa wanafunzi wa kigeni

11:50 - May 19, 2018
Habari ID: 3471519
TEHRAN (IQNA)- Chuo Kikuu cha Al Azhar nchini Misri kinapanga mashindano ya Qur'ani maalumu kwa wanachuo wa kigeni chuoni hapo.

Kwa mujibu wa taarifa, mashindano hayo yatajumuisha kuhifadhi na kusoma Qur'ani Tukufu na pia kutakuwa na kategoria za sanaa zitakazojumuisha mashairi  na kaligrafia ya Kiislamu.

Mashindano hayo ya Qur'ani yameandaliwa na Akademia ya Utafiti wa Kiislamu ya Al Azhar ambayo imesema moja ya malengo yake ni kutambua na kukua vipaji vya wanafunzi wa kigeni katika nyuga mbali mbali za Qur'ani, utamaduni na sayansi.

Katibu Mkuu wa taasisi hiyo Muhiddin Afifi amesema katika kategoria ya kuhifadhi Qur'ani, wanachuo watashindana katika kuhifadhi Qur'ani kikamilifu, kuhifadhi robo tatu, kuhifadhi Juzuu 15 na kuhifadhi robo moja. Ameongeza kuwa washiriki 10 bora katika kila shindano watapata zawadi.

Amesema baada ya mashindano hayo, wanachuo wataandaliwa kozi maalumu za kujiimarisha na kuboresha kiwango chao cha elimu ili waweze kuwa wawakilishi wanaostahiki wa Al Azhar katika nchi zao.

3715207

captcha