IQNA

Waislamu Ujerumani walalamikia undumakuwili wa Jimbo la Bavaria

19:03 - June 02, 2018
Habari ID: 3471540
TEHRAN (IQNA)- Waislamu nchini Ujerumani wameituhumu serikali ya jimbo la Bavaria kuwa ina sera za undumakuwili baada ya kuamuru idara zote za umma kuweka misalaba katika maeneo maalumu.

Markus Soeder, waziri mkuu wa Bavaria, ambaye ni kutoka chama chenye misimamo mikali ya Kikristo cha Christian Social Union (CSU), ametoa dikrii ya misalaba kuwekwa katika milango ya idara za serikali katika jimbo hilo.

Jambo ambalo limewakasirisha Waislamu ni kuwa, mwezi Machi mahakama ya jimbo la Bavaria iliwapiga marufuku wanawake Waislamu kuvaa Hijabu wakiwa mahakamani. Aiman Mazyek, Katibu Mkuu wa Baraza Kuu la Waislamu Ujerumani (ZMD) amesema, "sisi Waislamu hatuna tatizo na hiyo misalaba au kuheshimiwa dini katika jamii. Lakini serikali haipaswi kupendelea upande moja." Amesema kile ambacho hakikubaliki ni kuruhusu nembo za Ukristo na kupiga marufuku madhihiriso ya Uislamu au Uyahudi katika maeneo ya umma.

Naye Burhani Kesici pia amebanishwa mtazamo sawa na huo na kusema nembo na thamani za kidni ni muhimu katika jamii lakini akaongezwa kuwa, "kupiga marufuki Hijabu na wakati huo huo kuamuru misalaba iwekwe katika maeneo ya umma ni undumakuwili."

Kuna takribani Waislamu milioni nne nchini Ujerumani na hivyo kuufanya Uislamu kuwa dini ya pili kwa ukubwa nchini humo.

3465991

captcha