IQNA

Mshindi Mashindano ya Qur'ani nchini Somalia Azawadiwa Gari

14:23 - June 03, 2018
Habari ID: 3471542
TEHRAN (IQNA)- Mshindi katika Mashindano ya Kuhifadhi Qur'ani ya eneo la Somaliland nchini Somalia ametunukiwa zawadi ya gari.

Hamza Mohammoud Yasin ametunukiwa gari jipya aina ya Toyota Noah pamoja na kitita cha fedha baada ya kuibuka mshindi katika mashindano hayo katika sherehe iliyofanyika Jumapili.

Nafasi ya pili imechukuliwa na Ridwan Ahmed Farah wa mji wa Awdal ambaye ametunukiwa zawadi ya dola 1300 na laptopu. Hamza Osman Abdillahi na Samatar Nassir Hassan wamechukua nafasi za tatu na nne na kupata zawadi ya dola elfu 1000 na dola 700 kwa taratibu.

Mashindano ya mwaka huu ni ya sita kufanyika mfululizo katika Msikiti wa Ali Matan ambapo mfadhili wake ni Rais wa eneo la Somaliland Musa Bihi Abdi ambaye aliwatunuku washiriki zawadi. Rais Bihi amewapongeza vijana kwa ustadi wao na viwango vizuri vya kuhifadhi Qur'ani huku akibainisha matumaini yake kuwa vijana hao wataweza kutekeleza mafundisho ya Qur'ani maishani.

Waziri wa Masuala ya Dini na Wakfu Sheikh Khalil Abdillahi amemshukuru rais Bihi kwa kufadhili mashindano hayo na hivyo kuinua motisha na viwango vya elimu ya Kiislamu hasa kuhifadhi Qur'ani.

Eneo la Somaliland ilitangaza uhuru wake kutoka Somalia mwaka 1991, lakini halitambuliki na nchi yoyote ile wala Umoja wa Mataifa na linahesbiwa kuwa sehemu ya Jamhuri ya Kifiderali ya Somalia.

3720068

captcha