IQNA

Trump awapuuza Waislamu Wamarekani na kuwaalika mabalozi wa tawala za kiimla katika futari

17:33 - June 09, 2018
Habari ID: 3471549
TEHRAN (IQNA) - Jumatano iliyopita , Rais Donald Trump wa Marekani aliandaa katika Ikulu ya White House kile alichodai kuwa ni dhifa ya futari kwa ajili ya Waislamu, lakini la kushangaza ni kuwa Waislamu wa Marekani hawakualikwa.

Ikulu ya White House imekua ikiandaa dhifa za futari tokea utawala wa Clinton. Lakini mwaka huu, Rais Donald Trump ameandaa dhifa hiyo ya futari kwa mara ya kwanza katika utawala wake na kuibua utata mkubwa.

Hakuna viongozi wa Waislamu Marekani au wanaharakati Waislamu walioalikwa katika dhifa hiyo na badala yake ni mabalozi wa tawala vibaraka wa Marekani katika eneo la Masahriki ya Kati kama vile wawakilishi wa Saudi Arabia, Umoja wa Falme za Kiarabu na Jordan. Mmarekni pekee ambaye alionekana katika dhifa hiyo ya futari ni imamu katika Jeshi la Markeani. Ukulu ya White House imekataa kutoa orodha kamili ya watu walioalikwa na kuhudhuria dhifa hiyo ya futari ya Trump.

Taasisi kubwa za Wasialmu Marekani kama vile Baraza la Waislamu la Masuala ya Umma (MPAC) zimeshangaa ni kwa sababu gani hazikualikwa. "Hakuna jitihada yoyote iliyofanywa kuwaalika Waislamu kufnaya mazungumzo na Ikulu ya White House," amesema Hoda Hawa, mkurugenzi wa sera katika MPAC.

Kwa upande wake Baraza la Mahusiano ya Marekani na Uislamu (CAIR), ambalo hutetea haki za Waislamu, lilitangaa wazi kupinga dhifa hiyo ya futari ya Trump na kuandaa mjumuiko wa kuipinga nje ya Whote House.

Waandamanaji hao walipiga nara dhidi ya njama za Trump katika kuwapiga marufuku raia wa nchi kadhaa za Kiislamu kuingia Marekani sambamba na kuitaja hatua hiyo kuwa ya chuki na ya kibaguzi.

Katika futari hiyo ya kimaonyesho, Trump alikaa meza moja na Khalid bin Salman bin Abdulaziz Al Saud, mtoto wa Mfalme wa sasa wa Saudia na ambaye pia ni balozi wa Saudia nchini Marekani kadhalika Dina Kawar, balozi wa Jordan nchini Marekani. Kabla ya futari hiyo Colin Christopher mmoja wa viongozi wa ngazi za juu wa Jumuiya ya Kiislamu ya Amerika ya Kaskazini (ISNA) alituma barua pepe kwenda gazeti la Huffington Post la nchini Marekani akibainisha kwamba White House ilikuwa inapanga kuwaalika mabalozi wa nchi za kifisadi na ambazo zinakiuka haki za raia wake na Waislamu kushiriki futari hiyo.

3466023

captcha