IQNA

Idadi ya Wakenya wanaoelekea Hija yaongezeka

12:47 - August 01, 2018
Habari ID: 3471615
TEHRAN (IQNA)- Idadi ya Wakenya wanaoelekea Hija mwaka huu imeongezeka kwa waumini 800 ikilinganishwa na mwaka uliopita.

Baraza Kuu la Waislamu Kenya SUPKEM limetangaza kuwa mwaka huu kutakuwa na Waislamu 4,631 wanaotazamiwa kuelekea katika Ibada ya Hija.

Kwa mujibu wa SUPKEM, idadi hiyo ilikuwa ni 3,800 mwaka jana. Wakenya wanaoelekea Hija wanatazamiwa kuanza kuondoka nchini humo Agosti nne.

Wakati huo huo mwenyekiti wa SUPKEM, Balozi Yusuf Nzibo ametoa wito kwa wanaoelekea Hija kuhakikisha kujitayarisha kikamilifu kwa ajili ya safari hiyo huku akisisitiza ulazima wa kupata chanjo zote zinazohitajika, kuhakikisha wana pasi za kusafiria na visa  kabla ya kuanza safari. Ibada ya Hija mwaka huu inatazamiwa kufanyika baina ya Agosti 19-24 ambazo zinasadifiana na  7- 12 Dhul Hija mwaka 1439 Hijria Qamaria.

3735076

captcha