IQNA

Umoja wa Mataifa wakosoa hali ya Waislamu wa Rohingya nchini Myanmar

12:24 - August 23, 2018
Habari ID: 3471643
TEHRAN (IQNA)- Umoja wa Mataifa umeikosoa serikali ya Myanmar kwa kukwamisha juhudi zinazolenga kuwafikia Waislamu wa Rohingya katika jimbo la Rakhine wanaokabiliwa na hali mbaya.

Hayo yameelezwa na Knut Ostby, Mratibu wa Masuala ya Kibinadamu wa Umoja wa Mataifa Katika Masuala ya Myanmar na kusisitiza kwamba, ukwamishaji mambo huo wa serikali ya nchi hiyo umezorotesha juhudi zinazolenga kuwasaidia Waislamu hao.

Ameongeza kuwa, ofisi yake imekataa ombi la serikali ya Myanmar la kutembelea baadhi ya vijiji tu katika jimbo la Rakhine.

Hayo yanajiri katika hali ambayo, hivi karibuni Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Bangladesh ilifichua kwamba, serikali ya Myanmar imeitaka serikali ya nchi hiyo kusimamisha misaada ya kibinaadamu kwa malaki ya wakimbizi wa Rohingya walioko katika maeneo ya mpaka wa nchi mbili.

Wakati huo huo, ripoti mbalimbali za Umoja wa Mataifa zimekuwa zikieleza kwamba, jeshi la Myanmar limekuwa likifanya hujuma dhidi ya Waislamu Warohingya kwa shabaha ya kukiangamiza kizazi cha jamii hiyo ya Waislamu.

Wimbi jipya la jinai dhidi ya Waislamu Rarohingya  zilishika kasi tangu tarehe 25 mwezi Agosti mwaka jana. Hadi sasa  jinai hizo zimepelekea kuuliwa Waislamu zaidi ya elfu sita na kujeruhiwa maelfu ya wengine huku wengine karibu laki nano wakilazimika kuwa wakimbizi katika nchi jirani ya Bangladesh.

Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa Zeid Ra'ad Al Hussein amesema kuwa uhalifu unaofanywa na Mabudha kwa himaya ya serikali nchini Myanmar dhidi ya Waislamu wa jamii ya Rohingya ni mauaji ya kimbari.

Al Hussein anasisitiza kwamba, kuna udharura wa kufika katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo na kufanya uchunguzi kuhusu ukatili unaofanywa na serikali ya Myanmar dhidi ya Waislamu.

3740788

captcha