IQNA

Waislamu Mashia Saudia kushirikiana na vikosi vya usalama katika maadhimiso ya Ashura

12:01 - September 09, 2018
Habari ID: 3471664
TEHRAN (IQNA)- Sheikh Wajdi Mubarak mmoja katia ya wanazuoni wa Kishia nchini Saudi Arabia ametaka kuwepo ushirikiano kamili baina ya waumini na maafisa wa usalama nchini humo katika maadhimisho ya Siku ya Ashura.

Sheikh Mubarak ametuma ujumbe katika mitandao ya kijamii na kusema Waislamu wa madehebu ya Shia nchini Saudi Arabia wako tayari kaundaa maadhimisho ya kumbukumbu ya siku aliyouawa shahidi mjukuu wa Mtume Muhammad SAW, Imam Hussein AS, ambayo ni maarufu kama Siku ya Ashura. Amesisitiza kuhusu udharura wa wananchi kushirikiana na vikosi vya usalama vya Saudia katika kudumisha uslama siku hiyo. Mwanazuoni huyo wa Kishia nchini Saudia amesema maafisa wa usalama wana jukumu la kulinda usalama wa waumini wataoakoshiriki katika mijimuiko ya Siku ya Ashura nchini humo.

Sheikh Mubarak pia ametoa wito kwa maualmaa wote, wazungumzaji katika mimbar, wakuu wa Misikiti na kumbi za kidini zijulikanazo kama Husseiniya na wahusika wote wajitahidi kushirikiana ili kuandaa mijimuiko itakayofana katika Siku ya Ashura mwaka huu.

Halikadhalika ametoa wito kwa washiriki kuzingatia haki za wananchi wengine kama vile kutotumia sauti za juu zenye kukera, kuwa na nidhamu na unadhifu na kutofunga njia za magari na wapita njia wengine wakati wa a matembezi (masir) katika Siku ya Ashura. Inatazamiwa kwua Siku ya Ashura mwaka wa 1440 Hijria Qamaria itasadifiana na Alhamisi Septemba 20 2018 kwa kutegemea mwezi mwandamo.

Ikumbukwe kuwa, mwaka 61 Hijria Qamaria, moja kati ya vita mashuhuri katika historia ya Kiislamu na ya mwanadamu, vilitokea baina ya majeshi ya haki na batili katika ardhi ya Karbala huko Iraq.

Siku hii inajulikana kwa jina la Ashura. Katika siku hiyo mjukuu wa Mtume Muhammad SAW, Imam Hussein bin Ali bin Abi Twalib AS, alisimama kishujaa na wafuasi wake waaminifu 72, kukabiliana na jeshi kubwa la batili ili kuilinda dini ya Allah.

Katika siku kumi za kwanza za mwezi wa Muharram, Waislamu, hasa wafuasi wa Madhebu ya Shia na wale wawapendao Ahul Bayt wa Mtume SAW, hushiriki katika hafla mbali mbali za maombolezo ya Imam Hussein AS. Aidha hata wasio kuwa Waislamu katika maeneo mbali mbali pia hujumuika na Waislamu katika maombolezo ya Imam Hussein AS kwani aliuawa shahidi akitetea haki na kupinga udhalimu.

3745125

captcha