IQNA

13:53 - September 11, 2018
News ID: 3471667
TEHRAN (IQNA) - Msikiti mmoja umehujumiwa na kuharibiwa kaskazini magharibi mwa Ujerumani katika jimbo la Lower Saxony ambapo maandishi ya kibaguzi yamenadikwa katika kuta na nyama ya nguruwe kuachwa katika jengo la msikiti.

Hujuma hiyo imejiri Jumatatu katika Msikiti wa Selimiya katika mji wa Nordenham na polisi tayari wameshaanzisha uchunguzi kuhusu jinai hiyo.

Waliotekeleza hujuma hiyo pia waliandika maandishi ya kibaguzi katika madirisha na kutupa nyama ya nguruwe katika maeneo kadhaa ya msikiti huo.

Idris Aksut, mwanachama wa Jumuiya ya Msikiti wa Selimiye amesema hujuma hiyo ilijiri saa 10 alfajiri asubuhi na kuongeza kuwa wale wanaotaka kuwazuia Waislamu katika itikadi yao hawatafanikiwa.

Misikiti kadhaa imeshambuliwa nchini Ujerumani mwaka huu kutokana na ongezeko la chuki dhidi ya Uislamu nchini humo.

3466740

Name:
Email:
* Comment: