IQNA

Binti mwenye kuvaa Hijabu, taswira tafauti ya Waislamu wa Myanmar

Katika wimbi la habari za kusikitisha za jinai za Jeshi la Myanmar dhidi ya Waislamu wa jamii ya Rohingya nchini humo, binti mmoja Mwislamu mwanablogu amewasilisha taswira nyingine ya Waislamu wa nchi hiyo

Win Lae Phyu Sin ni binti Mwislamu mwenye umri wa miaka 19 na anaishi katika mji mkuu wa Myanmar, Yangon huku akijishughulisha na kazi yake ya kuuza vipodozi sambamba na kubainisha mapenzi na itikadi yake kwa vazi la Hijabu. Ana wafuatiaji zaidi ya 6000 katika Facebook na pia hadi sasa ametoa mafunzo kwa wanafunzi 600 katika darasa zake za utumizi wa vipodozi. Wanafunzi wa Phyu Shin wanasema anawapa ile hisia ya kujiamini na wanajifaharisha na utambulisho wao wa Kiislamu.