IQNA

Matembezi ya Siku ya Waislamu yafanyika New York

8:44 - September 25, 2018
Habari ID: 3471688
TEHRAN (IQNA)- Maelfu ya watu wameshiriki katika matembezi ya Siku ya Waislamu katika eneo la Manhattana mjini New York nchini Marekani.

Matembezi hayo ambayo yaliyofanyika Jumapili 23 Septemba ni ya 33 yalikuwa ya 33 yaifanyika kwa kauli mbiu ya ‘Rahma kwa Wote’. Mohammad Malik, mmoja kati ya viongozi wa jumuiya ya Kiislamu ya Muslim Majlis katika Kisiwa cha Staten amesema matembezi hayo yamelenga kuoneysha namna Waislamu wanavyofungamana na kueneza amani na kuwapenda wafuasi wa dini mbali mbali.

“Wanadamu wote ni wa Allah na hivyo tunaeneza ujumbe wa mapenzi,” Malik alisema wakati wa matembezi hayo.

Matembezi hayo yalianza kwa Sala ya Adhuhuri karibu na barabara ya Madison Avenue. Washiriki walibebe bendere za nchi zao zikiwemo Marekani, Nigeria, Pakistan, India n.k kwa lengo la kuoneysha kuwa Uislamu ni dini inayofuatwa na watu kutoka maeneo yote ya dunia.

Matembezi hayo yalifanyika kwa mara ya kwanza mwaka 1985 kwa lengo la kuleta umoja na kuwapa Waislamu Marekani uwezo wa kisiasa. Hatahivyo idadi ya washiriki imekuwa ikididimia kutokana na tatizo la chuki dhidi ya Uislamu nchini Marekani hali ambayo imekuwa mbaya zaidi baada ya kuchaguliwa Donald Trump ambaye anatekeleza rasmi sera ya kuwabagua Waislamu.

3466818

captcha