IQNA

Kampeni ya "Muhammad SAW, Mtume wa Walimwengu" yazinduliwa Brazil

8:08 - November 20, 2018
Habari ID: 3471746
TEHRAN (IQNA) – Jumuiya ya Taasisi za Kiislamu Brazil imezindua kampeni yenye anuani ya "Muhammad SAW, Mtume wa Walimwengu" kwa lengo la kumuarifisha Mtume Mtukufu wa Uislamu.

Jumuiya hiyo imesema inazinduia kampeni hiyo ambayo imependekezwa na Wizara ya Wakfu ya Misri. Kama sehemu ya kampeni hiyo, Jumuiya ya Taasisi za Kiislamu Brazil imesema itasambaza vitabu la lugha ya Kireno kuhusu Sirah ya Mtume Muhammad SAW. Aidha jumuiya hiyo imepanga kuandaa sherehe za Maulid ya Mtume SAW katika misikiti iliyo chini yake.

Kampeni ya "Muhammad SAW, Mtume wa Walimwengu" ni kampeni ya kimataifa ambayo imeanzishwa na Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kidini ya Misri kwa lengo la kumuarifisha Mtume Muhammad SAW kwa Walimwengu. 

Kampeni hiyo ni kwa mujibu wa Aya ya 107 ya Suuratul Anbiyaa katika Qur'ani Tukufu isemayo kuwa: "Nasi hatukukutuma ila uwe ni Rehema kwa walimwengu wote."

/3764365

captcha