IQNA

Kiongozi wa Hamas

Utawala wa Kizayuni ni adui mkuu wa Umma wa Kiislamu

18:11 - November 24, 2018
Habari ID: 3471750
TEHRAN (IQNA)-Kiongozi wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina, Hamas, amehutubu katika Kongamano la Kimataifa la Umoja wa Kiislamu mjini Tehran na kusema: "Utawala wa Kizayuni ni adui mkuu wa Umma wa Kiislamu."

Ameongeza kuwa: "Kadhia ya Palestina si kadhia ya kikaumu, chama au kundi bali ni kadhia ya umma wote wa Kiislamu. Akizungumza kwa njia ya video kutoka Ghaza katika sherehe za kufungua kongamano hilo mapema leo asubuhi, Ismail Haniya amesisitiza udharura wa kuuwekea vikwazo utawala wa Kizayuni. Aidha amesema ni jinai kuwa na uhusiano wowote wa kawaida na utawala wa Kizayuni wa Israel na kuongeza kuwa: "Taifa la Palestina katu halitakubali  njama ya  'muamala wa karne' itekelezwe.

Haniya amesisitiza kuwa, kupamabana dhidi ya Wazayuni maghasibu ni chanzo cha umoja wa umma wa Kiislamu na kuongeza kuwa: "Njama zote za Kuyahudisha ardhi ya Palestina hazitaweza kubadilisha ukweli wa kihistoria na kijiografia." Amesema Rais Donald Trump wa Marekani hana haki ya kumpatia adui Mzayuni hata chembe moja ya mchanga wa ardhi ya Palestina."

Mkuu wa Idara ya Kisiasa ya Hamas amesisitiza kuwa, mapambano ndio njia pekee ya kukomboa ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu. Ameongeza kuwa, pamoja na kuwepo changamoto nyingi ambazo maadui wameibua dhidi ya mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran lakini kongamano la kimataifa la umoja wa Kiislamu limefanyika Tehran na nukta hiyo inatoa bishara njema kuwa umma wa Kiislamu unaweza kuchukua hatua za kuelekea katika umoja pamoja na kuwepo changamoto zilizopo.

Mkutano wa 32 wa Kimataifa wa Umoja wa Kiislamu umeanza hapa mjini Tehran ukiwa umewakusanya pamoja washiriki 350 kutoka nchi 100 tofauti duniani.

Mkutano huo wa siku tatu umefunguliwa leo Jumamosi chini ya kaulimbiu ya "Quds, Mhimili wa Umoja Katika Ummah."

Mkutano huo hufanyika kila mwaka katika kipindi cha baina ya tarehe 12 na 17 Mfunguo Sita cha maadhimisho ya Maulidi na Siku ya Kuzaliwa Bwana Mtume Muhammad SAW na kinajulikana pia kwa jina la kipindi cha Wiki ya Umoja baina ya Waislamu.

/3766610/

captcha