IQNA

Uislamu ni dini pekee inayolinda haki zote za binadamu

15:19 - December 11, 2018
Habari ID: 3471767
TEHRAN (IQNA)- Washiriki wa warsha iliyofanyika hivi karibuni nchini Pakistan wamesema Uislamu ni dini pekee ambayo imeangazia kila kipengee cha maisha sambamba na kulinda haki za binadamu.

Katika warsha iliyofanyika Jumatatu mjini Mingora nchini  Pakistan chini ya anuani ya "Mtazamo wa Haki za Binadamu katika Uislamu na Magharibi", Lutfullah Saqib, Naibu Mkuu wa Kitengo cha Sheria katika Chuo Kikuu cha Swat alizungumza kuhusu nafasi ya Uislamu katika haki za binadamu na kulinganisha na ulimwengu wa Magharibi. Amesema nchi za Magharibi bado ziko mbali sana hadi kufikia kiwango bora cha haki za binadamu katika nyuga mbali mbali. Aidha alisema: "Uislamu ni dini bora zaidi na kwa mara ya kwanza katika historia ya mwanadamu dini hii ilibainishwa wazi kuhusu haki za binadamu katika sekta zote za maisha. Mtume Muhammad SAW katika hotuba yake ya mwisho alibainisha wazi kigezo cha haki za binadamu."

3467434

captcha