IQNA

Waislamu Nigeria wakumbuka mauaji ya Zaria

11:12 - December 14, 2018
Habari ID: 3471770
TEHRAN (IQNA)- Waislamu nchini Nigeria wanakumbuka mauaji ya umati yaliyotekelezwa na jeshi la nchi hiyo dhidi ya wafuasi wa Harakati ya Kiislamu Nigeria katika mji wa Zaria jimboni Kaduna.

Disemba mwaka 2015, Jeshi la Nigeria liliua kwa umati karibu wafuasi zaidi ya 1000 wa Harakati ya Kiislamu inayoongozwa na Sheikh Ibrahim Zakzaky wakiwemo wanawe watatu na baadaye kuwazika katika makaburi ya umati.

Kadhalika idadi kubwa ya wafuasi wa Sheikh Ibrahim Zakzaky walikamatwa wakati jeshi na vikosi vya ulinzi vya a vilipofanya jinai na ukandamizaji mkubwa dhidi ya ofisi za Harakati ya Kiislamu ya Nigeria (IMN)

Uvamizi huo ulijiri baada ya Jeshi la Nigeria kudai kuwa wafuasi wa Harakati ya Kiislamu walikuwa na njama ya kutaka kumuua mkuu wa jeshi hilo, madai ambayo yalikanushwa vikali na wafuasi wa harakati hiyo.

Tokea wakati huo Sheikh Zakzaky na mkewe wamekuwa wakizuiliwa katika mojawapo ya vituo vya kijeshi vya nchi hiyo bila kufunguliwa mashtaka. Maandamano yamekuwa yakifanyika kila mara kutaka Sheikh Zakzaku aachiliwe huru.

Wakati huo huo Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch limetoa mwito wa kufunguliwa mashitaka wanajeshi wa Nigeria wanaowakandamiza wanachama wa Harakati ya Kiislamu ambao aghalabu ni Waislamu wa madhehebu ya Shia.

Aniete Ewang, Mtafiti wa Human Rights Watch nchini Nigeria ametoa mwito huu Jumatano na kuongeza kuwa, kuendelea wimbi la unyanyasaji, ukandamizaji na kushambuliwa Waislamu wa madhehebu ya Shia nchini humo hakutakua na matokeo mengine ghairi ya kuvuruga zaidi hali ya usalama wa taifa nchini humo.

3467454

captcha