IQNA

Magaidi wa ISIS wameua wafungwa 700 Syria

11:58 - December 20, 2018
Habari ID: 3471778
TEHRAN (IQNA) Magaidi wakufurishaji wa kundi la ISIS (Daesh) wametekeleza mauaji mengine ya kutisha huko mashariki mwa Syria kwa kuua wafungwa mia saba karibu na eneo lililoko kwenye mpaka wa nchi hiyo na Iraq.

Shirika la Haki za Binadamu nchini Syria imeripoti kuwa, kundi hilo la ISIS limeua wafungwa wapatao mia saba katika kipindi cha miezi mwili karibu na mpaka wa nchi hiyo na Iraq.

Taasisi hiyo yenye makao yake makuu London huko Uingereza imesema wafungwa hao 700 walikuwa sehemu ya raia na wapiganaji 1350 waliokuwa wakishikiliwa na kundi la kigaidi la Daesh kandokandio ya mji wa Hajin.

Kundi la ISIS linadhibiti eneo dogo la ardhi ya mashariki mwa mto Furati (Euphrates) nchini Syria ambalo limevamiwa na wapiganaji wa kundi la Kikurdi la SDF linalopata himaya ya Marekani.

Eneo hilo limekuwa likishuhudia mapigano makali kwa miezi miwili sasa baina ya makundi hayo mawili.

Kiongozi wa kundi hilo la SDF amewaambia waandishi habari kwamba, wapiganaji wasiopungua elfu tano wa kundi la kigaidi la ISIS bado wapo katika eneo hilo na kwamba wengi wao ni raia wa kigeni ambao wako tayari kupigana hadi kufa.

Hayo yanajiri wakati ambao hivi karibuni Vikosi vya ulinzi vya Iraq vilitangaza habari ya kusambaratishwa timu nyingine ya mabaki ya magaidi huko magharibi mwa mji wa al Ramadi, makao makuuu ya mkoa wa al Anbar.

Kwa mujibu wa shirika la habari la AlSumaria News la nchini Iraq, idara ya usalama wa kijeshi ya nchi hiyo imetangaza habari hiyo leo na kuongeza kuwa, jeshi la Iraq limefanikiwa kusambaratisha timu hiyo ya magaidi saba wa ISIS katika wilaya ya Hiit ya mkoa wa al Anbar, magharibi mwa nchi hiyo.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa, magaidi hao walikuwa wakifanya shughuli zao kwa siri na walikuwa wanajiandaa kufanya shambulio la kigaidi dhidi ya wananchi wa Iraq.

3467504

captcha