IQNA

Trump amteua adui wa Uislamu kuwa mshauri wake

21:42 - January 18, 2019
Habari ID: 3471810
TEHRAN (IQNA)- Mashirika ya kutetea haki za raia nchini Marekani yamemlaani rais Donald Trump wa nchi hiyo kwa kumteua mtu mwenye chuki dhidi ya Uislamu kuwa naibu mshauri wa usalama wa taifa.

Hivi karibuni, Trump alimteua Charles M Kupperman kuwa msaidizi wa Mshauri wa Usalama wa Taifa John Bolton. Alipokuwa akimuarifisha, Trump alimtaja Kupperman kuwa mtu aliye na uzoefu wa miongo mine ykatika amsuala ya sera za usalama wa taifa.

Kupperman alikuwa mmoja kati ya wakurugenzi wa Kituo cha Sera za Usalama (CSP) baina yam waka 2001 na 2010. Mashirika ya kijamii Marekani yanasema CSP ni kundi lenye chuki dhidi ya Uislamu kutokana na sera zake za kueneza nadharia kuwa Waislamu wanalenga kuiteka Marekani.

Baraza la Mahusiano ya Kiislamu Marekani, CAIR, ambalo hutetea haki za Waislamu nchini humo, limemtaka Trump abatilishe uteuzi wa Kupperman. Mkuu wa masuala ya serikali katika CAIR, Rober McCaw amesema hatua ya Trump kumteua Kupperman ni mfano wa wazi wa kuwaweka watu wenye chuki dhidi ya Uislamu kusimami usalama wa taifa.

Katika kampeni zake za urais mwaka 2016, Trump alitaka Waislamu wapigwe marufuku kikamilifu kuingia nchini humo.

Baada ya kuingia madarakani Trump alitia saini amri ya kuwazuia kutoka nchi kadhaa kuingia nchini humo licha ya upinzani mkubwa dhidi ya uamuzi huo.

Amri hiyo imawazuia au kuwawekea vizingiti Waislamu kutoka nchi za Iran, Libya, Somalia, Sudan, Syria na Yemen kuingia Marekani.

3467722

captcha