IQNA

Bustani ya kale zaidi ya miche ya ua la Nargis* katika mkoa wa Khuzestan, kusini maghairbi mwa Iran, imekuwepo kwa muda wa miaka 4,000 katika mji mdogo wa Behbahan. Kila mwaka katika msimu wa majira ya baridi kali huanza shughuli ya kuvuna maua ya Nargis na kuupa mji huo mazingira ya machipuo. Wakuu wa Behbahan wanasema takribani maua milioni 34 hadi milioni 40 ya Nargis huvunjwa katika mji huo. *Kisayansi ua la Nargis linajulikana kama Narcissus na malenga wa Kiingereza wanaliita daffodil