IQNA

Msingi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran ni Qur'ani Tukufu

14:43 - February 04, 2019
Habari ID: 3471829
TEHRAN (IQNA) – Msemaji wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (IRGC) amesisitiza kuwa msingi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran ni Qur'ani Tukufu.

Akizungumza na IQNA, Brigedia Jenerali Ramadhan Shariff amesema mapinduzi ya Kiislamu yameenea katika eneo kutokana na kuwa msingi wake ni Qur'ani Tukufu.

Amesema kabla ya Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran mwaka 1979, kulikuwa na kambi mbili za idiolojia duniani ambapo moja iliyokuwa ya Kikomunisti ikiongozwa na Shirikisho la Soviety ya zamani na nyingine ilikuwa ya uliberali ambayo ingali inaongozwa na Marekani.

Amesema baada ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu, idiolojia ambayo msingi wake ni Qur'ani Tukufu na Sunna ya Mtume Muhammad SAW ilienea duniani.

Aidha amesema mafanikio ya Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran katika kipindi cha miaka 40 iliyopita yametokana na utekelezwaji wa mafundisho ya Qur'ani. Amesema ili mafanikio hayo yaweze kuendelea kuna aja ya kuendelea kusimama imara katika utekeelzwaji wa mafundisho ya Qur'ani.

Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran yaliongozwa na Hayati Imam Khomeini MA ambaye alianzisha mfumo mpya ya kisiasa uliojengeka katika msingi wa thamani za Kiislamu na kura za wananchi.

Tokea yapate ushindi Mapinduzi ya Kiislamu, harakati za Qur'ani zimeimarika kote Iran.

Febrauru 11, 2019 kutakuwa na sherehe kubwa nchini Iran na maeneo mengine duniani kuadhimisha mwaka wa 40 wa ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu.

3786939

captcha