IQNA

Taifa la Iran laadhimisha miaka 40 ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu

22:33 - February 11, 2019
Habari ID: 3471837
TEHRAN (IQNA)- Mamilioni ya wananchi Waislamu wa Iran wamejitokeza kwa wingi kushiriki katika maandamano ya kuadhimisha miaka 40 ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu.

Katika msimu huu wa baridi kali ambao huandamana na mvua na theliuji, Wairani wamejitokeza kwa wingi katika maandamano hayo kote nchini, kudhihirisha utiifu wao kwa malengo ya Mwasisi Mkuu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Khamenei. 

Maandamano ya leo ya maadhimisho ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya mwaka huu yamefanyika katika miji zaidi ya elfu moja na vijiji elfu kumi vya Iran ya Kiislamu.

Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran yalifikia kilele cha ushindi tarehe 11 mwezi Februari mwaka 1979 kwa uongozi wa Imam Khomeini (M.A), Mwasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Februari 11 miaka 40 iliyopita Iran ilikuwa katika siku ya kihistoria itakayokumbukwa siku zote, ambapo  wananchi wanamapinduzi wa Iran, wanaume kwa wanawake, vijana kwa wazee na watu wa matabaka yote walisimama kidete wakipambana na mizinga na vifaru vya jeshi la Shah na kujisabilia kwa ajili ya Mapinduzi ya Kiislamu.

Akihutubu Katika sherehe za ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu katika Medani ya Azadi (Uhuru) mjini Tehran, Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema nchi hii haiombi na wala haitaomba ruhusa kwa mtu yeyote ya kuunda aina mbali mbali za makombora na zana za ulinzi; na itaendelea kufuata njia yake kwa nguvu na uwezo kamili.

Rais Rouhani amesisitiza kwa kusema: Dunia nzima ijue kwamba, nguvu na uwezo iliona Jamhuri ya Kiislamu ya Iran leo hii ni mkubwa zaidi mara kadhaa kuliko ilivyokuwa katika zama za Kujihami Kutakatifu; na vikosi vya ulinzi vya Iran vinajitosheleza katika uundaji wa anuai za silaha na zana za kijeshi.

Rais Rouhani ameashiria ujasiri na moyo wa ushujaa vilionao vikosi vya ulinzi katika kuilinda nchi na kueleza kwamba: Walimwengu wameona jinsi wananchi wa Syria, Iraq na Lebanon walivyopata ushindi kutokana na irada na msaada wa Iran; na huko Palestina na Yemen pia muqawama wa kukabiliana na maghasibu na wavamizi ungali unaendelea.

Rais wa Iran amesisitiza kuwa: Leo maadui wamelazimika kukiri kuwa wameshindwa katika uingiliaji wao wa miaka 20 katika eneo na kuanza kuondoka kidogo kidogo ili mataifa ya eneo hili yaweze kuendeleza kwa uhuru njia yao ya ustawi na maendeleo.

Rais Rouhani pia Rouhani ameashiria maendeleo iliyopata Iran katika nyuga mbali mbali ikiwemo ya petrokemikali na kueleza kwamba: Dunia nzima inakiri kuhusu maendeleo ya kasi iliyopata Iran. Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amebainisha kwamba, kuwa na nafasi Uislamu, wananchi yaani Jamhuri na kufanyika chaguzi za kuwachagua viongozi ni miongoni mwa matunda na mafanikio muhimu ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

3789135

captcha