IQNA

18:26 - March 01, 2019
News ID: 3471857
TEHRAN (IQNA)- Ripoti ya Umoja wa Mataifa imebaini kuwa yamkini utawala haramu wa Israel umetenda jinai za kivita au jinai dhidi ya binadamu katika oparesheni zake za kijeshi zinazowalenga Wapalestina katika Ukanda wa Ghaza

Ripoti iliyotolewa Alhamisi  na wataalamu wa Umoja wa Mataifa imesema, ushahidi unaonesha kuwa utawala wa Israel ulifanya jinai dhidi ya binadamu au jinai za kivita wakati wa kukabiliana na maandamano ya amani ya mwaka 2018 ya Wapalestina katika eneo la Ukanda wa Ghaza.

Ripoti hiyo imesema kuwa, walenga shabaha wa jeshi la Israel walikuwa wakiwapiga risasi kwa makusudi watoto wadogo, wafanyakazi wa uokoaji na waandishi wa habari waliokuwa katika maandamano hayo ya Ghaza.

Mkuu wa tume ya uchunguzi ya Umoja wa Mataifa kuhusu matukio ya Ukanda wa Gaza, Santiago Canton pia ametoa taarifa akisema askari wa Israel wamekiuka sheria za kimataifa za haki za binadamu na sheria za kibinadamu. Canton  amesisitiza kuwa, uhalifu huo unatambuliwa kuwa ni jinai dhidi ya binadamu.

Timu hiyo ya wataalamu wa Umoja wa Mataifa imekusanya ripoti ya jinai dhidi ya binadamu zilizofanywa na walenga shabaha na makamanda wa jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel ambayo imekabidhiwa kwa Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa, Michelle Bachelet.

Tangu tarehe 30 Machi mwaka jana Wapalestina wa Ukanda wa Gaza wamekuwa wakifanya maandano yaliyopewa jina la Haki ya Kurejea katika kila siku za Ijumaa. Maandamano hayo hufanyika katika mpaka wa Ukanda wa Ghaza na ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu (Israel).  Tangu wakati huo jeshi la Israel limekuwa likishambulia maandamano hayo ya amani na hadi sasa limeua raia wasiopungua 260 wa Palestina na kujeruhi wengine wasiopungua elfu 27.

Wakati huo huo, Jumuiya ya Nchi za Kiarabu, Arab League, imeunga mkono ripoti ya hiyo ya Umoja wa Mataifa kuhusu jinai ambazo zinatendwa na utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Wapalestina katika Ukanda wa Ghaza. Saeed Abu Ali, Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu na amesema: "Ripoti ya Umoja wa Mataifa kuhusu jinai za utawala wa Kizayuni dhidi ya Wapalestina imetayarishwa kwa mujibu wa sheria za kimataifa.

3468026

Name:
Email:
* Comment: