IQNA

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu asisitiza kuhusu kulinda mazingira+PICHA

12:50 - March 07, 2019
Habari ID: 3471866
TEHRAN (IQNA)- Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Khamenei amesisitiza umuhimu wa utunzaji misitu na kusema umuhimu wa kupanda miti ni jambo ambalo linapaswa kuhimizwa ili liwe utamaduni wa umma.

Ayatullah Khamenei aliyasema hayo Jumatano mjini Tehran wakati alipopanda miche miwili ya miti ya matunda katika bustani ya Ofisi ya Kiongozi Muadhamu kwa munasaba wa maadhimisho ya Wiki ya Maliasili na Siku ya Kupanda Miti nchini Iran. Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameongeza kuwa, siku hii ya kupanda miti ni nembo ambayo lengo lake ni la kuhimiza utamaduni wa kupanda miti na kuzuia uharibifu wa misitu. Akifafanua zaidi kuhusu ulazmia wa kulinda mazingira na kupanda miti, Kiongozi Muadhamu alisema: "Katika kulinda misitu kunapaswa kuwepo jitihada kubwa. Taasisi husika, kama vile vyombo vya Mahakama, zinapaswa kuchukua hatua zote  zinazotakiwa kuzuia kuharibiwa misitu. Ni matumaini yetu kuwa, kwa ustawi wa moyo wa kupenda miti na maeneo ya kijani kibichi, katika mustakabali nchi hii hii na watu wetu wataweza kufaidika na kadhalika Mwenyezi Mungu ataweza kuzidisha Baraka zitokanazo na mimea na mazingira ya kijani kibichi, Inshallah."

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu asisitiza kuhusu kulinda mazingira+PICHA

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu asisitiza kuhusu kulinda mazingira+PICHA

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu asisitiza kuhusu kulinda mazingira+PICHA

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu asisitiza kuhusu kulinda mazingira+PICHA

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu asisitiza kuhusu kulinda mazingira+PICHA

3468078/

captcha