IQNA

15:34 - March 10, 2019
News ID: 3471870
TEHRAN (IQNA)- Waislamu nchini Marekani wanabaguliwa zaidi ya wafuasi wa dini zingine zote nchini humo.

Kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa na Tovuti ya The Hii na HarrisX, asilimia 85 ya waliohojiwa wanaamini kuwa Waislamu Marekani wanabaguliwa huku asilimia 79 wakisema ni Mayahudi wanaobaguliwa. Asilimia 61 ya walioshiriki katika uchunguzi huo wanasema ni Wakristo wanaobaguliwa zaidi.

Uchunguzi huo wa maoni umechapishwa katika Ijumaa iliyopita baada ya Bunge la Marekani, Congress, kupitisha muswada wa kulaani chuki dhidi ya Uislamu, chuki dhidi ya Uyahudi na kila aina ya ubaguzi. Wabunge watatu Waislamu katika bunge hilo wamepongeza kupitishwa muiswada huu wakiutaja kuwa wa kihistoria.

"Ni mara ya kwanza katika historia ya nchi yetu kupigwa kura ya kulaani chuki dhidi ya Uislamu," walisema wajumbe Ilhan Omar, Rashida Tlaib na Andre Carson katika taarifa yao ya pamoja. Wabunge hao watatu ni wa chama cha Democrat.

Muswada huo umepigiwa kura baada  Bi.Omar kukosoa ushawishi hasi wa utawala haramu wa Israel  nchini Marekani jambo ambalo liliibua hasira miongoni mwa watetezi wa utawala huo ambao walidai matamshi yake ni sawa na chuki dhidi ya Uislamu.

Msimamo wa Omar wa kuukosoa utawala wa Kizayuni wa Israel kutokana na jinai zake dhidi ya Wapalestina pamoja na ushawishi wa lobi za Kizayuni katika siasa za Marekani umemfanya akabiliwe na uadui na kuandamwa na hujuma za viongozi na wanasiasa mbalimbali, akiwemo rais wa nchi hiyo Donald Trump ambaye ni maarufu kwa chuki zake dhidi ya Waislamu.

3468092

Name:
Email:
* Comment: