IQNA

13:28 - March 11, 2019
News ID: 3471871
TEHRAN (IQNA) – Waziri wa Elimu wa Iran Sayyid Mohammad Bathayi amesema takribani wanafunzi zaidi ya milioni mbili nchini Iran wanashiriki darsa za kuhifadhi Qur'ani.

Akizungumza katika, katika hafla ya kuwaenzi washindi wa Mashindano ya Qur'ani hivi karibuni katika mji wa Qum, alisema hivi sasa wanafunzi milioni 2.2 katika shule za msingi na upili wanashiriki katika masomi ya kuhifadhi Qur'ani. Amepongeza hatua ya kuandaliwa mashindano ya Qur'ani katika shule za Qur'ani na kusema husaidia kuimarisha ufahamu wa Qur'ani miongoni mwa wanafunzi.

Mwaka 2011, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Sayyid Ali Khamenei alishauri kuwa kunapaswa kuchukuliwa hatua za kuhakikisha vijana milioni 10 wanahifadhi Qur'ani kikamilifu nchini Iran. Aliagiza taasisi husika za Qur'ani nchini kuanzisha, Mpango wa Kitaifa wa Kuhifadhi Qur'ani ili kuwezesha Wairani milioni 10 wahifadhi Qur'ani.

Tokea ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran mwaka 1979, kumeshuhudiwa ongezeko kubwa la harakati za Qur'ani hapa nchini Iran na mojawapo ni mashindano ya kimataifa ya Qur'ani ambayo hufanyika kila mwaka.

3468104

Name:
Email:
* Comment: