IQNA

Msafara wa Rahian-e Noor (Wasafiri wa Nuru)* wanachuo wa kigeni katika Chuo Kikuu cha Tehran ukiwa na wanachuo 150 wa kike na kiume kukutoka nchi za Lebanon, Uturuki, Argentina, Senegal, Nigeria, Kodivaa, Italia, Afghanistan wametembelea maeneo ya oparesheni za kivita kusini mwa Iran kama vile Huweizeh, Talaeiyeh, Shalamche na Hoor al -Azim kwa muda wa siku nne.

*Msafara wa Wasafiri wa Nuru ,maarufu kama Rahian-e Noor nchini Iran, ni msafara wa watu wa matabaka mbali mbali ya jamii ambao hutembelea maeneo ambayo yalikuwa medani ya mstari wa mbele wa vita kusini na kusini magharibi mwa Iran wakati wa vita vya kujihami kutakatifu. Vita hivyo vilivyoendelea kwa muda wa miaka minane vilianza baada ya utawala wa Kibaath wa Iraq kuihujumu Iran mwaka 1980. Maeneo yanayotembelewa huwa na kumbukumbu za zama za vita zikiwemo kumbukumbu za mashahidi waliouawa katika vita hivyo vitakatifu vya kujihami.