IQNA

Kiongozi wa Hizbullah Hassan Nasrallah

Trump amezitusi nchi za Kiislamu, Kiarabu kwa kuitambua miinuko ya Golan kuwa milki ya Israel

13:20 - March 27, 2019
Habari ID: 3471890
TEHRAN (IQNA)-Katibu Mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon amesema kuwa, hatua ya Rais Donald Trump wa Marekani ya kuitambua rasmi miinuko ya Golan kuwa ni miliki ya utawala bandia wa Israel ni kuzitusi na kuzivunjia heshima nchi za Ulimwengu wa Kiislamu na Kiarabu.

Sayyid Hassan Nasrallah amesema hayo  jana Jumanne mjini Beirut, Lebanon alipohutubu kwa njia ya televisheni kuhusu masuala ya kitaifa na kienei. Kiongozi wa Hizbullah aliashiria hatua ya kihasama na kiuadui ya  Rais Donald Trump dhidi ya miinuko ya Golan inayokaliwa kwa mabavu na Israel na kubainisha kuwa, hatua hiyo ya Washington dhidi ya miinuko ya Golan, ni pigo kubwa kwa mchakato wa amani katika eneo la Magharibi mwa Asia (Mashariki ya Kati).

Katibu Mkuu wa Hizbullah ameashiria safari ya Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Marekani Mike Pompeo nchini Lebanon na kusema kuwa, katika safari yake hiyo, hakutoa matamshi yoyote ya nia safi ambayo yanatabikiana na ukweli wa mambo nchini Lebanon, bali alichokifanya ni kutoa matamshi yaliyojaa mjumuiko wa uwongo dhidi ya Iran na Hizbullah.

Sayyid Nasrallah amesisitiza kuwa, katika kipindi cha miaka 34 iliyopita, Harakati ya Hizbullah imelitetea na kulilinda taifa la Lebanon na akaongeza kusema kwamba, inachotakka Marekani ni kuimarisha uvamizi wa utawala wa Kizayuuni wa Israel na kulifanya taifa la Lebanon likabiliwe na hatari.

Aidha amesisitiza kuwa, Iran iko pamoja na Hizbullah kwa ajili ya kuhakikisha nchini Lebanon kunapatikana amani na uthabiti wa kudumu.

Jumatatu ya juzi Donald Trump alitekeleza vitisho vyake, kwa kusaini eti azimio la kuitambua miinuko ya Golan ya Syria kuwa mali ya utawala wa Kizayuni wa Israel, hatua ambayo imeendelea kukosolewa katika kila kona ya dunia.

Kiongozi wa Hizbullah pia ametahadharisha kuwa, baada ya Marekani kutambua Quds Tukufu (Jeruslem) kuwa mji mkuu wa utawala wa Israel, na sasa hatua yake ya kutmabua miinuko ya Golan ya Syria kuwa  milki ya Israel, ni wazi kuwa mtawala huyo wa Mareknai sasa analenga kutambua Ukingo wa Maghribi wa Mto Jordan kuwa milki ya utawala ghasibu wa Israel. Amesema nchi za Kiarabu zikiendelea kunyamaza kimya mtawala huyo wa Marekani ataambua eneo hilo muhimu la Palestina kuwa milki ya utawala wa Kizayuni wa Israel. Aidha Sayyid Nasrallah amesema mapambano na muqawama ndio njia pekee ya kuzikomboa ardhi za Palestina, Syria na Lebanon zinazokaliwa kwa mabavu na utawala ghasibu wa Israel.

3468193

captcha