IQNA

Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ya Malaysia yamalizika

11:54 - April 23, 2019
Habari ID: 3471926
TEHRAN (IQNA) – Mashindano ya 61 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Malaysia yalimalizika Jumamosi usiku kwa kutunukiwa zawadi washindi.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, washindi walitangazwa na kutunukiwa zawadi katika sherehe iliyofanyika mjini Kuala Lumpur na kuhudhuriwa maafisa wa ngazi za juu pamoja na wanazuoni.

Kwa mujibu wa matokeo yaliyotangazwa na jopo la majaji, qarii wa nchi mwenyeji, Malaysia, Ahmad Khair bin Jalil alishika nafasi ya kwanza katika kitengo cha qiraa akifuatiwa na wawakilishi wa Algeria na Morocoo huku mwakilishi wa Iran Hadi Mowahid Amin akishika nafasi ya nne.

Katika kitengo cha kuhifadhi Qur'ani, mshindi alikuwa ni Mohammad Abdu wa Sweden akifuatiwa na Mohammad Marouf Hussain na Canada huku Haitham Sagar Ahmad wa Kenya akishika nafasi ya tatu.

Katika mashindano ya wanawake kitengo cha qraa, mshindi alikuwa Nur Farahtul Firuzi Panut wa Malaysia na katika katika kitengo cha kuhifadhi mshindi alikuwa ni Asiya Othman Jibril Mohammad wa Algeria.

Mashindano ya 61 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Malaysia yalifanyika kati ya Aprili 16-20 ambapo kulikuwa na washiriki 107 kutoka nchi 71. Mashindano hayo ya Malaysia ni maarufu kama Majlis Tilawa al-Qur'an.

3805095

captcha