IQNA

Iran yasitisha kwa muda utekelzwaji baadhi ya vipengee vya mapatano ya nyuklia ya JCPOA

14:08 - May 08, 2019
Habari ID: 3471946
TEHRAN (IQNA) -Iran imesimamisha kwa muda utekelezaji wa baadhi ya ahadi zake kuhusu mapatano ya nyuklia ya Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelezwaji (JCPOA), ikiwa ni mwaka mmoja baada ya Marekani kujitoa kwa upande mmoja katika mapatano hayo muhimu ya kimataifa.

Iran tayari imeshazifahamisha rasmi nchi tano zilizosalia katika mapatano hayo ya nyuklia ya mwaka 2015 kuhusiana na uamuzi wake wa

Leo Jumatano mabalozi wa nchi tano hizo yaani Ufaransa, Uingereza, Ujerumani, Russia na China mjini Tehran wamekabidhiwa barua iliyoandikwa na Rais Hassan Rouhani wa Iran kuhusiana na uamuzi huo muhimu. Barua hiyo imekabidhiwa mabalozi hao na Abbas Araqchi, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran.

Aidha leo Jumatano Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa Iran imesimamishwa kwa muda wa siku 60 uuzaji nje wa urani yake iliyorutubishwa pamoja na maji mazito.

Ikitangaza habari hiyo leo mchana Mei 8 ikiwa ni mwaka mmoja baada ya Marekani kujitoa kinyume cha sheria katika mapatano ya kimataifa ya nyuklia mashuhuri kama Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelezaji JCPOA, na kukanyaga azimio nambari 2231 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, Rais Hassan Rouhani amesema kwamba Iran imezifahamisha nchi tano zilizosalia katika mapatano hayo kwamba Iran haitauza tena nje urani hiyo iliyorutubishwa pamoja na maji yake mazito. Amesema Iran imeziambia nchi wanachama wa mapatano hayo ambazo ni Uingereza, Ufaransa, Ujerumani, Russia na China kuwa zina muhula wa siku 60 ili zirejee kwenye meza ya mazungumzo.

Amesema iwapo nchi hizo zitarejea kwenye mazungumzo na kuidhaminia Iran maslahi yake mahimu na hasa kuhusiana na sekta ya mafuta na benki, basi Iran itarejea tena katika hali iliyokuwepo kabla ya kusimamisha mauzo hayo ya urani na maji mazito la sivyo, itachukua hatua nyingine iwapo nchi hizo hazitakuwa zimetoa jibu la kuridhisha katika kipindi hicho cha siku 60. Rais Rouhani amesema: Iran ilikubali katika mapatano ya JCPOA kusimamisha urutubishaji wake wa urani katika kiwango cha 3.67 lakini sasa hatutatekeleza jambo hilo kwa maana kwamba hatuna kiwango maalumu cha kufikisha urutubishaji wetu. Ama kuhusiana na tanuri la maji mazito lililoko Arak pia, baada ya kumalizika siku 60, tutaamua kurejea katika ratiba yetu ya kabla ya kufikiwa mapatano ya JCPOA na kulikanilisha tanuri hilo la maji mazito.

Rais Rouhani amesema: Kwa mara nyingine tumezitahadharisha nchi tano zilizosalia katika mapatano ya JCPOA kwa kuziambia wazi kwamba iwapo zitaichukulia hatua yetu ya leo kama kisingizio cha kutaka kulirejesha faili la Iran katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, zitakabiliwa na hatua kali na madhubuti zaidi. Rais Rouhani amesema hakuna wakati wowote ambao Iran imeanzisha vita lakini kwamba haitakubali kuburuzwa.

3809847

captcha