IQNA

Dunia yajitayarisha kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Quds

12:31 - May 25, 2019
Habari ID: 3471971
TEHRAN (IQNA) – Waislamu na wasiokuwa Waislamu kote duniani wanajitayarisha kudhimisha Siku ya Kimataifa ya Quds (Jerusalem) kwa lengo la kutangaza kufungamana kwao na malengo ya ukombozi wa ardhi za Palestina ambazo zinakaliwa kwa mabavu na utawala wa Kizayuni wa Israel.

Aidha katika siku hiyo ya Quds washiriki katika maandamano na vikao mbali mbali hulaani jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel na uungaji mkono wa Marekani kwa utawala huo ghasibu.

Mwasisi wa Jamhuri ya Kiislamu hayati Imam Khomeini (Mwenyezi Mungu amrehemu) ndiye aliyeipa siku hiyo ya Ijumaa ya mwisho ya mwezi Ramadhani jina la Siku ya Kimataifa ya Quds kwa shabaha ya kuakisi dhulma ya kihistoria inayofanywa na madola ya Magharibi yanayodai kutetea haki za binadamu, dhidi ya watu wanaoendelewa kudhulumiwa na kukandamizwa wa Palestina na ardhi yao takatifu. Tokea ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran mwaka 1979, Siku ya Kimataifa ya Quds imekuwa ikiadhimishwa kote duniani.
Suala la kukombolewa Palestina kutoka kwenye makucha ya Wazayuni maghasibu lilikuwa miongoni mwa malengo na kaulimbiu kuu za Imam Ruhullah Khomeini tangu alipoanza harakati zake hapo mwaka 1960. Wakati huo Imam alikutaja kuasisiwa dola haramu la Israel katika ardhi ya Palestina kuwa ni kitendo cha kishetani na kuutaja utawala huo kuwa ni tezi ya saratani ambalo inapaswa kuondolewa na kukatwa kwa njia yoyote ile inayowezekana.

Mwaka huu, Siku ya Kimataifa ya Quds inasadifiana na Ijumaa Mei 31.

3468596

captcha