IQNA

Mashindano ya Qur'ani nchini Uswisi

14:13 - June 10, 2019
Habari ID: 3471992
TEHRAN (IQNA) – Mashindano ya Qur'ani yamefanyika nchini Uswisi kwa himaya ya Jumuiya ya Kimataifa la Al Raham ya nchini Kuwait.

Kwa mujibu wa mwandalizi wa mashindano hayo Bw. Jamal al Khateeb, hayo ni mashindano ya kwanza ya aina yake ya Qur'ani kufanyika katika nchi hiyo ya Ulaya.

Kwa ujumla watu 50 kuanzia miaka saba hadi sabini wameshiriki katika mashindano hayo ya kusoma na kuhifadhi Qur'ani yaliyokuwa na makundi matano tafauti.

Mshindi wa kila kundi ametunukiwa zawadi ya safari ya Umrah.

Al Khateen amesema mashindano kama hayo yanawapa motisha Waislamu nchini humo kusoma na kuhifadhi Qur'ani Tukufu.

3818036

 

captcha