IQNA

Kongamano la Pili la Kimataifa la Vijana wa Muqawama (mapambano ya Kiislamu) limefanyika Jumatatu 24 Juni na kuhudhuriwa na Ayatullah Sheikh Isa Qassim, Kiongozi wa Mashia wa Bahrain, Hujjatul Islam wal Muslimin Hashim Al Haidary, Mkuu wa Masuala ya Utamaduni katika Harakati ya Hashdu Shaabi ya Iraq, Ayatullah Ali Ridha Arafi, Mkuu wa Vyuo vya Kidini vya Iran, Ayatullah Abbas Kaabi, Mwanachama wa Baraza la Wanazuoni Wanaomchagua Kiongozi Muadhamu nchini Iran, Hujjatul Islam wal Muslimin Ali Abbasi, Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Al Mustafa (SAW), wanazuoni, wanafunzi wa vyuo vya kidini na watu wa matabaka mbali mbali.

Kongamano hilo lilifanyika katika mkesha wa kongamano dhidi ya Palestina na Ushia ambalo lilifanyika Bahrain katika fremu ya mpango wa 'Muamala wa Karne'. Kongamano la Pili la Kimataifa la Vijana wa Muqawama limefanyika katika ukumbi wa Ghadir wa Idara ya Kuhubiri Uislamu ya Vyuo Vikuu vya Kidini (Hawza).